// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAGERA SUGAR KUWAKOSA FAKHI, KAVILLA NA KIBAYA MECHI NA AZAM IJUMAA CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAGERA SUGAR KUWAKOSA FAKHI, KAVILLA NA KIBAYA MECHI NA AZAM IJUMAA CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, September 13, 2017

  KAGERA SUGAR KUWAKOSA FAKHI, KAVILLA NA KIBAYA MECHI NA AZAM IJUMAA CHAMAZI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kagera Sugar ya Bukoba itawakosa wachezaji wake watatu majeruhi, mabeki Jaffar Kibaya, Mohammed Fakhi na kiungo na Nahodha, Geogre Kavilla katika mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Azam FC Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime Kianga ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo baada ya timu yake kuwasili mjini Dar es Salaam jana kwamba anasikitika kuwakosa nyota wake hao watatu kuelekea mchezo huo mgumu wa ugenini.
  Mohammed Fakhi (kulia) atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Azam FC Ijumaa kwa sababu ni majeruhi

  “Tumeingia jana na leo tunafanya mazoezi Uwanja wa Karume na kesho tutapumzika kwa ajili ya mechi ya keshokutwa dhidi ya Azam FC kule Chamazi na majeruhi ni wachezaji watatu  Jaffar, Fakhi na Kavila, ambao waliumia wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu,” amesema Mexime.
  Mexime amesema anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu, lakini wamejipanga kwenda Azam Complex kupambana ili wapate ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu msimu huu.
  “Ligi ni ngumu kwa kweli na mchezo wa keshokutwa utakuwa mgumu kwa sababu Azam ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri na sisi tumejipanga kufanya vizuri japo tumeanza vibaya,”amesema.
  Kagera Sugar itaingia katika mchezo wa Ijumaa ikitoka kuambulia pointi moja tu katika mechi mbili za nyumbani, baada ya kufungwa 1-0 na Mbao FC ya Mwanza Agosti 28 kabla ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Septemba 10 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR KUWAKOSA FAKHI, KAVILLA NA KIBAYA MECHI NA AZAM IJUMAA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top