// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RUVU SHOOTING YAFUATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU KWA LIPULI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RUVU SHOOTING YAFUATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU KWA LIPULI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, September 13, 2017

  RUVU SHOOTING YAFUATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU KWA LIPULI

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Ruvu Shooting kinatarajia kuondoka nchini kesho kwenda mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Lipuli FC Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora uliopo mkoani Iringa.
  Ruvu Shooting waliuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu baada ya kufungwa mabao 7-0 na Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Agosti 26, mwaka huu kabla ya kwenda kulazimisha sare ya 1-1 na Kagera Sugar mjini Bukoba mwishoni mwa wiki.
  Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wachezji wote wana hali nzuri na leo wanaendelea na mazoezi kwenye  Uwanja wao wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani kabla ya safari yao kesho.
  “Tunamshukuru Mungu tunaendelea vizuri japokuwa matokeo yanatuumiza, tunakiri kuwa tumeanza Ligi vibaya na timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wetu uliopo Mabatini na naimani tutafanya vizuri dhidi ya Lipuli siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa na tunatarajia kuondoka kesho asubuhi kuelekea mkoani humo kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Lipuli,”amesema Bwire
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAFUATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU KWA LIPULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top