// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GYAN AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO SIMBA IKIWAPIGA 5-0 HARD ROCK - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GYAN AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO SIMBA IKIWAPIGA 5-0 HARD ROCK - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, September 03, 2017

  GYAN AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO SIMBA IKIWAPIGA 5-0 HARD ROCK

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya Mghana wa Simba, Nicholas Gyan amefunga bao lake la kwanza leo timu yake ikiendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa mabao 5-0 Hard Rock ya Pemba katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Gyan aliyesajiliwa mwezi uliopita kutoka ya kwao Ghana, alifunga bao la tatu dakika ya 47, baada ya Mohammed ‘Mo’ Ibrahim kufunga mawili dakika ya 10 na 38.
  Mabao mengine ya Wekundu wa Msimbazi katika mchezo wa leo yamefungwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 57 na Said Ndemla dakika ya 59.
  Nicholas Gyan amefunga bao lake la kwanza leo Simba ikiibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Hard Rock ya Pemba


  Simba inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Marius Omog ilicheza vizuri leo na kuizidi kabisa uwezo Harrd Rock inayomilikiwa na Jeshi la Zanzibar.
  Kwa Simba, mchezo wa leo ulikuwa sehemu ya maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Septemba 9, Uwanja wa Uhuru pia.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Emmanuel Mseja, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Ally Shomary, Yussuf Mlipili, Paul Bukaba, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Jamal Mwambeleko dk63, James Kotei, Laudit Mavugo, Juma Luizio/Nicholas Gyan dk46 na Mwinyi Kazimoto.
  Hard Rock; Nelson Kimath, Gidion William/Rashidi Kawambwa dk50, Mussa Mude/Maulid Juma dk50, Emmanuel Balele, Joseph Simon/Juma Masele dk70, Ally Sapi, Salum Hassan, Hamisi Thabit, Ally Kenya, Hamisi Pacha na Hamisi Shango.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GYAN AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO SIMBA IKIWAPIGA 5-0 HARD ROCK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top