• HABARI MPYA

  Thursday, February 29, 2024

  RAIS MSTAAFU ALHAJ MWINYI AFARIKI DUNIA


  RAIS Mstaafu na aliyekuwa mpenzi wa michezo, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam akiwa ana umri wa miaka 98 baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda.
  Mwinyi aliyezaliwa Mei 8, mwaka 1925 eneo la Kivure, mkoani Pwani alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka Novemba 5 mwaka 1985 akichukua nafasi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi Novemba 23 mwaka 1995 alipomuachia madaraka, Benjamín William Mkapa, wote marehemu.
  Awali alikuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar kuanzia Januari 30 mwaka 1984 akichukua nafasi ya Aboud Jumbe Mwinyi hadi Oktoba 24 mwaka 1985 alipomuachia Idris Abdul Wakil, wote marehemu pia.
  Enzi za uhai wake, Mwinyi alikuwa mpenzi wa michezo aliyehudhuria matukio mengi ya michezo ukiwemo mchezo wa marudiano wa Fainali Kombe la CAF baina ya Simba SC na Stella Adjamé ya Ivory Coast Novemba 27 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Simba ilifungwa 2-0 ikitoka kutoa sare ya bila mabao Novemba 14 Jijini Abidjan.
  Baada ya mchezo huo, Alhaj Mwinyi alikasirishwa na matokeo hayo na kusema; Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu’ kwenye michezo ambacho kila mmoja anajifunzia kunyoa.
  Alhaj Mwinyi alihudhuria mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga na Coffee ya Ethiopia Mei 9 mwaka 1998 Uwanja huo huo wa Taifa kabla ya kubadilishwa jina na kuwa Uhuru.
  Yanga ilishinda 6-1 na kufuzu Robó Fainali iliyochezwa kwa mfumo wa makundi kwa ushindi wa jumla wa 8-3, kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 26 Jijini Addis Ababa.
  Baada ya mchezo huo, Alhaj Mwinyi kwa furaha akasema añafuta kauli yake ya Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kwenye michezo.
  Kwenye Sanaa, utamaduni na burudani Alhaj Mwinyi aliunga mkono pia na inakumbukwa mwaka 1992 alimpokea Mfalme wa muziki wa PoP, Mmarekani Michael Jackson ‘Wacko Jacko’ naye marehemu pia katika ziara yake nchini na wakafanya mazungumzo.
  Pumzika kwa amañi Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amín.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS MSTAAFU ALHAJ MWINYI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top