HII ndio ratiba ya michuano ya Ngao ya Jamii inayotarajiwa kuanza Agosti 9 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga ikishirikisha mabingwa watetezi, Yanga SC, Simba SC, Azam FC na Singida Fountain Gate.
Yanga itafungua dimba na Azam FC Agosti 9, kabla ya Simba SC kucheza na Singida Fountain Gate Agosti 10 na washindi watakutana katika Fainali Agosti 13, mchezo ambao utatanguliwa mechi ya kusaka mshindi wa Tatu hapo hapo Mkwakwani.
0 comments:
Post a Comment