// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWENYEKITI WA SIMBA SC AHUDHURIA KOZI YA FIFA AUSTRALIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWENYEKITI WA SIMBA SC AHUDHURIA KOZI YA FIFA AUSTRALIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, August 16, 2023

  MWENYEKITI WA SIMBA SC AHUDHURIA KOZI YA FIFA AUSTRALIA


  MWENYEKITI wa Bodi ya Simba SC, Salim Abdallah Muhene 'Try Again' amehudhuria kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika jijini Sydney, Australia.
  Akiwa huko, Try Again amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino kuhusu Africa Super League na ushiriki wa Simba kwenye michuano hiyo pamoja na kuzungumzia mambo mengi yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na hasa Tanzania.
  Rais Infantino amepongeza hatua kubwa ya maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na zaidi Tanzania. 
  Ameipongeza pia Tanzania kwa kazi kubwa ambayo inafanyika katika kukuza mpira akifurahishwa zaidi Simba na vilabu vingine chini ya usimamizi mzuri wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI WA SIMBA SC AHUDHURIA KOZI YA FIFA AUSTRALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top