• HABARI MPYA

  Friday, August 04, 2023

  TANZANIA YATWAA UBINGWA WA CECAFA U18 WANAWAKE


  TANZANIA imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 18 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Tanzania katika mchezo huo limefungwa na Winfrida Gerlad dakika ya 42 na kwa ushindi huo wanamaliza na pointi 12, tatu zaidi ya Uganda baada ya michezo yote minne ya michuano hiyo.
  Jumla ya timu tano zilishiriki michuano hiyo, nyingine Ethiopia iliyomaliza na pointi sita nafasi ya tatu, Burundi nafasi ya nne pointi tatu huku Zanzíbar ambayo haikuvuna pointi ikimaliza mkiani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YATWAA UBINGWA WA CECAFA U18 WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top