Ligi Kuu itaanza Agosti 15, mwaka huu, mabingwa watetezi, Yanga wakifungua dimba na KMC Agosti 23 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Watani wao, Simba wataanzia Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro Agosti 17, huku Azam FC wakianzia nyumbani Azam Complex dhidi ya Tabora United Agosti 16.
Azam FC watacheza kwanza na Yanga Oktoba 25 kabla ya kumenyana na Simba SC Novemba 28 mechi zote zikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment