• HABARI MPYA

  Sunday, August 27, 2023

  SINGIDA YACHAPWA 2-0 NA JKU LAKINI YASONGA MBELE AFRIKA


  TIMU ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ imefanikiwa kwenda hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya JKU leo yamefungwa na Nassor Juma dakika ya saba na Gamba Matiko dakika ya 42 na kwa matokeo hayo Singida Big Stars inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia kushinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita na sasa watamenyana na Future ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA YACHAPWA 2-0 NA JKU LAKINI YASONGA MBELE AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top