TIMU ya Arsenal imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Nottingham Forest jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Arsenal jana yalifungwa na Eddie Nketiah dakika ya 26 na Bukayo Saka dakika ya 32, kabla ya winga wa zamani wa Manchester United, Anthony Elanga kumsetia Taiwo Awoniyi kuwapa bao la kufutia machoziNottingham Forest dakika ya 82.
0 comments:
Post a Comment