• HABARI MPYA

  Sunday, August 20, 2023

  YANGA SC YAWACHAPA ASAS 2-0 CHAMAZI


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, ASAS ya Djibouti katika mchezo wake wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na wachezaji wake wa kigeni, kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 22 na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda dakika ya 53.
  Timu hizo zitarudiana Agosti 26 hapo hapo Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWACHAPA ASAS 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top