• HABARI MPYA

  Sunday, August 20, 2023

  AZAM FC YACHAPWA 2-1 NA BAHIR DAR LEO ETHIOPIA


  TIMU ya Azam FC imefungwa Mabao 2-1na wenyeji, Bahir Dar katika mchezo wake wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa, Ethiopia.
  Mabao yote ya Bahir Dar yamefungwa na Fitsum Gebremariam dakika ya 20 na 60, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji wa wake Mkongo, Idris Ilunga Mbombo dakika ya 72.
  Timu hizo zitarudiana Agosti 25 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na Club Africain ya Tunisia kuwania kuingia hatua ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 2-1 NA BAHIR DAR LEO ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top