JANA jioni Yanga SC ilicheza mechi ya kirafiki na kutoka sare ya bila kufungana na JKU ya Zanzibar Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima kwa jana pekee kwa Yanga baada ya asubuhi kuibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Friends Rangers.
Kwa ujumla Yanga imecheza mechi nne za kujiandaa na msimu chini ya kocha mpya, Muargentina Miguel Angel Gamondi, nyingine mbili ikishinda 1-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na 10-0 dhidi ya Magereza ya Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment