TIMU ya Singida Fountain Gate imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa LITI mjini Singida.
Katika mchezo wa kuhitimisha tamasha la Singida Bid Day, mabao ya wenyeji yamefungwa na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika 20 na winga mzawa, Dickson Ambundo dakika ya 43, wakati la AS Vita limefungwa na Ngoma Manianga dakika ya tatu.
0 comments:
Post a Comment