• HABARI MPYA

  Tuesday, August 22, 2023

  ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 1-0 BAO LA TUTA EMIRATES


  WASHINDI wa Ngao ya Jamii, Arsenal wameshinda mechi ya pili mfululizo ya Ligi Kuu ya England baada ya usiku wa jana pia kuwalaza wenyeji, Crystal Palace 1-0 Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Bao pekee la Washika Bunduki hao limefungwa na kiungo Mnorway, Martin Odegaard kwa penalti dakika ya 53 kufuatia kipa Sam Johnstone kumchezea faulo Eddie Nketiah kwenye boksi.
  Lakini Arsenal ilimaliza pungufu mchezo huo kufuatia Takehiro Tomiyasu kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 67.
  Ikumbukwe mechi ya kwanza Vijana wa Mikel Arteta waliichapa Nottingham Forest 2-1 Uwanja wa Emirates, wakati Crystal Palace ilianza na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Sheffield United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 1-0 BAO LA TUTA EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top