• HABARI MPYA

  Thursday, August 31, 2023

  SINGIDA YATOA SARE NYINGINE NYUMBANI 0-0 NA TABORA UNITED


  TIMU ya Singida Fountain Gate imelazimishwa sare ya bila kufungana na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Ni sare ya pili mfululizo Singida ‘ The Big Stars’ wanatoa, tena za bila mabao katika mechi mbili za mwanzo za msimu nyumbani baada ya kutoka suluhu pia na Tanzania Prisons kwenye mechi ya kwanza.
  Kwa upande wao Tabora United, zamani Kitayosce leo wameokota pointi ya kwanza ya Ligi kufuatia kufungwa mabao 4-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA YATOA SARE NYINGINE NYUMBANI 0-0 NA TABORA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top