• HABARI MPYA

  Saturday, August 19, 2023

  NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE YA 1-1 KWA KMC RUANGWA


  TIMU ya Namungo imecheza mechi ya pili nyumbani ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara bila ushindi baada ya leo kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  KMC walitangulia na bao la Rashid Chambo dakika ya 69, kabla ya mshambuliaji Mkongo, Fabrice Ngoye kuisawazishia Namungo FC kwa penalti dakika ya 80.
  Huu ulikuwa mchezo wa kwanza katika msimu mpya kwa KMC, wakati Namungo mechi yao ya kwanza walifungwa 1-0 na JKT Tanzania hapo hapo Majaliwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE YA 1-1 KWA KMC RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top