• HABARI MPYA

  Saturday, August 26, 2023

  ARSENAL YAPUNGUZWA KASI, SARE 2-2 NA FULHAM EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wamelazimishwa ya sare ya kufungana mabao 2-2 na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka kwa penalti dakika ya 70 na Eddie Nketiah dakika ya 72, wakati ya Fulham iliyomaliza pungufu baada ya beki Mnigeria, Calvin Bassey kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa mbili za njano - yamefungwa na Andreas Pereira dakika ya kwanza na Joao Palhinha dakika ya 87.
  Arsenal inafikisha pointi saba katika mechi tatu za mwanzo za msimu kufuatia awali kushinda zote mbili, wakati Fulham inafikisha ponti nne baada ya awali kufungwa moja na kutoa sare moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPUNGUZWA KASI, SARE 2-2 NA FULHAM EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top