• HABARI MPYA

  Wednesday, August 30, 2023

  SABA YANGA WAITWA TAIFA STARS, SIMBA WANNE, AZAM…


  WACHEZAJI saba wa klabu bingwa ya Tanzania, Yanga SC wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast dhidi ya Algeria Septemba 7 Jijini Algiers.
  Watani wao, Simba wametoa wachezaji wanne, huku Azam FC ikitoa wachezaji mmoja tu.
  Taifa Stars itamenyana na Algeria Septemba 7 Uwanja wa Mei Venue Stade du 19, 1956 Annaba ikihitaji ushindi ili kufuzu AFCON.
  Kwa sasa Algeria ambayo imekwishafuzu inaongoza Kundi F kwa pointi 15, ikifuatiwa a Tanzania yenye pointi saba, wakati ina pointi nne mbele ya Níger wanaoshika mkia kwa pointi zao mbili.
  Uganda itamaliza na Níger siku hiyo hiyo, Septemba 7 Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.
  Tanzania imefuzu AFCON mara mbili tu kihistoria, mwaka 1980 nchini Nigeria na mwaka 2009 nchini Misri.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SABA YANGA WAITWA TAIFA STARS, SIMBA WANNE, AZAM… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top