• HABARI MPYA

  Saturday, August 26, 2023

  RAHEEM STERLING APIGA MBILI CHELSEA YASHINDA 3-0


  TIMU ya Chelsea imepata ushindi wa kwanza chini ya kocha Muargentina, Mauricio Pochettino baada ya kuichapa Luton Town FC mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya The Blues yalifungwa na washambuliaji Muingereza Raheem Sterling, mawili dakika ya 17 na 68 na Mgambia Nicolas Jackson dakika ya 75.
  Chelsea inafikisha pointi nne katika mchezo wa tatu kufuatia sare ya 1-1 na Liverpool Agosti 13 hapo hapo Stamford Bridge na kichapo 3-1 kutoka kwa West Ham United Agosti 20 Uwanja wa London.
  Kwa upande wao Luton Town FC wanapokea kipigo cha pili mfululizo wakitoka kufungwa 4-1 na Brighton & Hove Albion Agosti 12 Uwanja wa The Amex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAHEEM STERLING APIGA MBILI CHELSEA YASHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top