• HABARI MPYA

  Thursday, August 03, 2023

  TANZANIA NA CUBA KUSHIRIKIANA KATIKA MCHEZO WA NGUMI


  TANZANIA kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali ya Cuba kupitia Taasisi ya INDER ya nchini humo zimekubaliana kushirikiana katika eneo la kuendeleza mchezo wa ngumi.
  Taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kwamba mabondia wa Tanzania watapata fursa ya kuweka Kambi Cuba ambayo pia itatoa makocha kuja kufundisha ngumi nchini na kubadilishana ujuzi.
  Makubaliano hayo yamefikiwa jana, Agosti 2, 2023 wakati Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ alipofanya mazungumzo na Raul Fornes Valenciano ambaye ni  Makamu wa Rais wa kwanza wa Taasisi hiyo ya Kitaifa ya Michezo, Elimu na Burudani ambacho ni chombo kinachohusika na ukuzaji wa michezo, elimu ya viungo na burudani nchini Cuba.
  Taasisi hiyo  tayari ina mashirikiano na baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Algeria ambapo hubadilishana uzoefu kwenye eneo la mchezo wa ngumi.
  Naibu Waziri Mwinjuma yupo nchini Cuba kwa ajili ya kuhudhuria maonesho ya kimataifa ya michezo ya Havana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA NA CUBA KUSHIRIKIANA KATIKA MCHEZO WA NGUMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top