• HABARI MPYA

  Wednesday, August 02, 2023

  UGANDA YAJIWEKA PAZURI UBINGWA CECAFA MABINTI U18


  UGANDA jana ilijiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati kwa mabinti chini ya umri wa miaka 18 baada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Burundi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mechi nyingine ya jana, Ethiopia waliishindilia Zanzibar mabao 6-1 hapo hapo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanaifanya Uganda ipande kileleni kwa pointi zake tisa, sawa na Tanzania lakini yenyewe inakaa juu kwa wastani wa mabao kuelekea mechi ya kuamua bingwa baina yao Ijumaa.
  Mchezo wa Ijumaa Tanzania inatakiwa tu kushinda, lakini ikiwa sare Uganda watakuwa mabingwa kwa wastani mzuri wa mabao yao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA YAJIWEKA PAZURI UBINGWA CECAFA MABINTI U18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top