• HABARI MPYA

  Thursday, August 10, 2023

  SIMBA SC YAIFUATA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII


  TIMU ya Simba imefanikiwa kwenda Fainali ya Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Pongezi kwa kipa namba moja wa Simba kwa sasa, Ally Salim aliyepangua shuti la Aziz Andambwile, kabla ya Yussuf Kagoma kupiga juu ya lango, huku penalti za Singida zikifungwa na viungo Mtogo Marouf Chekei na Mkenya Duke Abuya.
  Waliofunga penalti za Simba ni viungo raia wa Msumbiji, Luis Miquissone, Mrundi, Saido Ntibanzokiza, mzawa Muzamil Yassin na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri na sasa Wekundu wa Msimbazi watakutana na mtani, Yanga katika Fainali Jumapili Saa 1:00 usiku hapo hapo Mkwakwani.
  Ikumbukwe Yanga ilitangulia Fainali jana baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC, mabao ya kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na mshambiliaji mzawa, Clement John Mzize dakika ya 89.
  Singida Fountain Gate na Azam FC zitamenyana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kuanzia Saa 9:00 Alasiri hapo hapo Mkwakwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIFUATA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top