• HABARI MPYA

  Sunday, August 27, 2023

  NUNEZ ATOKEA BENCHI DAKIKA ZA JIONI KUIBEBA LIVERPOOL


  TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Newcastle United leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Venue St. James' Park, Newcastle upon Tyne.
  Newcastle United walitangulia na bao la Anthony Gordon dakika ya 25, kabla ya Liverpool kupata pigo kufutia beki wake, Virgil van Dijk kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 28.
  Shujaa wa Liverpool leo ni Darwin Nunez aliyetokea benchi dakika ya 77 na kufunga mabao yote dakika ya 81 na 90 na ushei huo ukiwa ushindi wa pili katika mechi tatu, nyingine wakitoa sare.
  Newcastle United baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao tatu za mechi tatu sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NUNEZ ATOKEA BENCHI DAKIKA ZA JIONI KUIBEBA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top