• HABARI MPYA

  Saturday, August 26, 2023

  MAN UNITED YATOLA NYUMA KWA 2-0 NA KUSHINDA 3-2


  WENYEJI, Manchester United wametoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa  Old Trafford Jijini Manchester.
  Nottingham Forest ilitangulia kwa mabao ya Taiwo Awoniyi dakika ya pili na Willy Boly dakika ya nne, kabla ya Manchester United kuzinduka kwa mabao ya Christian Eriksen dakika ya 17, Casemiro dakika ya 52 na Bruno Fernandes dakika ya 76 kwa penalti.
  Hata hivyo, Nottingham Forest wanaobaki na pointi zao tatu za mechi tatu - walimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki Joseph Adrian Worrall kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 67 na kwa ushindi huo Man United wanafikisha pointi sita katika mchezo wa tatu pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOLA NYUMA KWA 2-0 NA KUSHINDA 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top