• HABARI MPYA

  Monday, August 28, 2023

  AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA PRISONS 3-1


  TIMU ya Azam FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 11 na wazawa Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 47 na Nathaniel Chilambo dakika ya 82, wakati la Prisons limefungwa na Zabona Khamis dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi sita sawa na Simba, lakini wanakaa kileleni kwa wastani mzuri wa mabao, wakati Prisons inabaki na pointi yake moja baada ya wote kucheza mechi mbili mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA PRISONS 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top