• HABARI MPYA

  Friday, August 18, 2023

  SINGIDA STARS YAITANDIKA JKU 4-1 KOMBE LA SHIRIKISHO CHAMAZI


  TIMU ya Singida Fountain Gate ‘Big Stars’ imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusogea mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKU ya Zanzibar usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Singida Fountain Gate leo yamefungwa na viungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya nne na 39 yote kwa penalti, Mnigeria Maurice Chukwu dakika ya 44 na Duke Abuya dakika ya 47, wakati la JKU limefungwa na Saleh Abdullah kwa penalti pia dakika ya 63.
  Timu hizo zitarudiana Agosti 27 hapo hapo Azam Complex na mshindi wa jumla atamenyana na Future ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA STARS YAITANDIKA JKU 4-1 KOMBE LA SHIRIKISHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top