• HABARI MPYA

  Wednesday, August 16, 2023

  FEISAL APIGA HAT TRICK AZAM YAICHAPA KITAYOSCE 4-0


  WENYEJI, Azam FC wameanza vyema Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kitayosce ya Tabora usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 18 tu, mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah matatu dakika za tatu, tisa na 13 huku lingine likifungwa na Prince Dube Mpumelelo dakika ya tano.
  Sababu za mechi hiyo kuishia dakika ya 18 ni Kitayosce kubaki na wachezaji watano uwanjani baada ya wawili kati ya saba walioanza kuumia, hivyo kwa mujibu wa kanuni refa akamaliza mchezo.
  Kitayosce ililazimika kuanza na wachezaji saba tu baada ya wengine wote kutokuwa na leseni za kuwaruhusu kucheza.
  VIDEO: HAT TRICK YA FEISAL DHIDI YA KITAYOSCE
  VIDEO: BAO LA PRINCE DUBE V KITAYOSCE
  VIDEO: UFAFANUZI WA BODI YA LIGI MECHI KUVUNJWA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FEISAL APIGA HAT TRICK AZAM YAICHAPA KITAYOSCE 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top