• HABARI MPYA

  Friday, August 25, 2023

  AZAM FC YATOLEWA KWA MATUTA KOMBE LA SHIRIKISHO


  TIMU ya Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 3-3 na Bahir Dar ya Ethiopia leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Dakika 90 za leo zilimalizika kwa Azam FC kushinda 2-1 na kufanya sare ya jumla ya 3-3 baada ya Bahir Dar kushinda 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa.
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya kwanza na Prince Dube dakika ya 10, wakati la Bahir Dar limefungwa na Habtamu Tadesse dakika ya 17.
  Katika mikwaju ya penalti kipa Mghana wa Azam FC, Idrissou Abdulai aliokoa penalti mbili za Bahir Dar.
  Upande wa Azam FC waliofunga ni Yanick Bangala, Feisal Salum na Cheikh Sidibe, wakati Sospeter Bajana, Idris Mbombo na Djibril Sylla wote wamekosa na kwa matokeo hayo, Bahir Dar itamenyana na Club Africain ya Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATOLEWA KWA MATUTA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top