• HABARI MPYA

  Saturday, August 19, 2023

  LIVERPOOL YAICHAPA BOURNEMOUTH 3-1 ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool inayofundishwa na Kocha Mjerumani, Jurgen Klopp yamefungwa na Luis Diaz dakika ya 27, Mohamed Salah dakika ya 36 na Diogo Jota dakika ya 62 katika mchezo ambao kiungo wake Muargentina, Alexis Mac Allister alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 58
  Bao pekee la Bournemouth lilifungwa na mshambuliaji Mghana, Antoine Semenyo dakika ya tatu hicho kikiwa kipigo cha kwanza kwao msimu huu baada ya sare ya 1-1 nyumbani na West Ham United, huku Liverpool ikifikisha pointi nne baada ya sare ya 1-1 ugenini na Chelsea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA BOURNEMOUTH 3-1 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top