• HABARI MPYA

  Friday, August 04, 2023

  GRACE MWAKAMELE AINGIA FAINALI NDONDI AFRIKA BAADA YA KUMDUNDA MSENEGAL


  BONDIA wa kike, Mtanzania Grace Joseph Mwakamele amefanikiwa kuingia Fainali ya michezo ya Ngumi za Ridhaa Afrika baada ya ushindi wa pointi dhidi ya Seynabou Ndiaye wa Senegal uzito wa Light Middle leo Jijini Yaounde, Cameroon.
  Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania, Lukelo Willilo, sasa Grace ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufika hatua hiyo, kesho katika Fainali atapambana na Alicida Panguane wa Msumbiji ambaye ni Bingwa mtetezi.
  Mtanzania mwingine, Yusuf Changalawe ameingia Nusu Fainali upande wa wanaume na atazipiga na Nathan Mbeli Langu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Konho (DRC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRACE MWAKAMELE AINGIA FAINALI NDONDI AFRIKA BAADA YA KUMDUNDA MSENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top