• HABARI MPYA

  Sunday, August 20, 2023

  MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA COASTAL UNION MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Unión ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Coastal Union walitangulia kwa bao la Ibrahim Ajibu dakika ya 70, kabla ya Kassim Haruna ‘Tiote’ kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 84, kila timu ikiokota pointi ya kwanza ndani ya mechi mbili baada ya wote kupoteza mechi za kwanza.
  Wakati Mtibwa Sugar ilifungwa 4-2 na Simba SC hapo hapo Manungu, kwa upande wao Coastal Unión walichapwa 2-1 na wenyeji, Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA COASTAL UNION MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top