• HABARI MPYA

  Saturday, August 12, 2023

  MWENYEKITI WA ZAMANI SIMBA, CHAMSHAMA AFARKKI DUNIA INDIA


  ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Simba SC, Ayubu Saleh Chamshama amefariki dunia jana (Agosti 11, 2023) hospitalini nchini India alipokuwa anafanyiwa matibabu.
  Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Soud Ayubu Chamshama msiba upo nyumbani kwake Chang’ombe, Maduka Mawili na mazishi yatafanyika Jumanne (Agosti 15, 2023) kijijini kwao Kilole, Lushoto, Mkoani Tanga.
  Pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Simba SC miaka ya 1980, enzi za uhai wake Chamshama pia alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya Majani ya Chai (Tanzania Tea Blenders),  na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke.
  Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ayoub Saleh Chamshama. Amin.
  Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI WA ZAMANI SIMBA, CHAMSHAMA AFARKKI DUNIA INDIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top