• HABARI MPYA

  Sunday, August 06, 2023

  AZAM FC YAICHAPA KMKM 4-0 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, KMKM katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na wachezaji wake wapya, kiungo Mgambia Djibril Sylla na mshambuliaji Msenegal,Alassane Diao huku mengine mawili KMKM wakijifunga wenyewe.
  Huo unakuwa mchezo wa pili kwa Azam FC tangu irejee kutoka Tunisia ilipoweka kambi ya kujiandaa na msimu baada ya jana kuifunga Bandari ya Mombasa nchini Kenya mabao 2-0 hapo hapo Azam Complex.
  Na ulipo kuwa Tunisia, Azam FC ilicheza mechi nne, ikifungwa mbili, 3-0 na Esperance 3-1 na Stade Tunisien na kushinda mechi mbili, 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan na 2-1 dhidi ya wenyeji wengine, US Monastir.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA KMKM 4-0 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top