• HABARI MPYA

  Sunday, August 13, 2023

  NI AZAM FC WASHINDI WA TATU NGAO YA JAMII, SINGIDA CHALI MKWAKWANI


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya timu nne ya Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na nyota wake, mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya kwanza na kiungo chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Abdul Suleiman Sopu dakika ya 42.
  Azam iliangukia kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu baada ya kufungwa 2-0 na Yanga kwenye mchezo wa Nusu Fainali Jumatano, wakati Singida Fountain Gate ilitolewa kwa penalti 4-2 na Simba baada sare ya bila kufungana hapo hapo Mkwakwani.
  Mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii utafuatia Saa 1:00 usiku hapo hapo Uwanja wa Mkwakwani baina ya Simba na Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI AZAM FC WASHINDI WA TATU NGAO YA JAMII, SINGIDA CHALI MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top