• HABARI MPYA

  Tuesday, August 15, 2023

  DODOMA JIJI WANG’ARA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU NYUMBANI


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Unión katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwa Dodoma Jiji, kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya Coastal Unión kutangulia na bao la dakika ya 46 Hijja Ugando, kabla ya wenyeji hao kuzinduka kwa mabao ya kipa Justin Ndikumana aliyejifunga dakika y 54 na Meshack Abraham dakika ya 60.
  Dodoma Jiji wanakuwa wenyeji pekee leo kupata ushindi katika mechi za kwanza za msimu baada ya Ihefu kufungwa 1-0 Geita Gold Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya na Namungo FC kuchapwa 1-0 pia na JKT Tanzania Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI WANG’ARA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top