• HABARI MPYA

  Sunday, August 20, 2023

  SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 UHURU


  WASHINDI wa Ngao ya Jamii, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa Dodoma Jiji FC mabao 2-0 leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji wake wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke dakika ya 43 na Mzambia, Moses Phiri dakika ya 55 huo ukiwa ushindi wa pili mfululizo ndani ya michezo miwili ya mwanzo baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 4-2 Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top