• HABARI MPYA

  Tuesday, August 29, 2023

  MAX NZENGELI APIGA MBILI YANGA YAUA 5-0 TENA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuitandika JKT Tanzania mabao 5-0 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na nyota wake wa kigeni, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 45 na ushei, Mzambia Kennedy Musonda dakika ya 54, Muivory Coast Kouassi Attohoula Yao dakika ya 64 na Mkongo Max Mpia Nzengeli mawili, dakika ya 79 na 88.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi sita na kupanda kileleni ikizizidi wastani wa mabao Azam FC na Simba SC baada ya wote kucheza mechi mbili, wana Jangwani wakijiwekea rekodi ya kipekee kuvuna mabao 10 kwenye mechi mbili. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAX NZENGELI APIGA MBILI YANGA YAUA 5-0 TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top