• HABARI MPYA

  Sunday, August 27, 2023

  JKT QUEENS YATINGA FAINALI KLABU AFRIKA MASHARIKI NA KATI WANAWAKE


  TIMU ya JKT Queens imefanikiwa kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Katí baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Burundi leo Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha FUFA, Njeru nchini Uganda.
  Mabao ya JKT Queens yamefungwa na Donisia Minja, Stumai Abdallah na Winfrida Gerlad, wakati bao pekee la la Abuja Queens limefungwa na Teopostar Situma.
  Sasa JKT Queens itakutana na mshindi kati ya CBE F.C.  ya Ethiopia Vihiga Queens FC ya Kenya zinazomenyana hivi sasa katika Fainali ambayo itapigwa Jumatano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT QUEENS YATINGA FAINALI KLABU AFRIKA MASHARIKI NA KATI WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top