• HABARI MPYA

  Monday, August 21, 2023

  WEST HAM YAICHAPA CHELSEA 3-1 LONDON


  WENYEJI, West Ham United wameitandika Chelsea mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London Jijini London.
  Mabao ya West Ham United yamefungwa na Nayef Aguerd dakika ya saba, Michail Antonio dakika ya 53 na Lucas Paqueta dakika ya 90 kwa penalti, wakati bao pekee la Chelsea limefungwa na Carney Chukwuemeka dakika ya 28.
  Ni ushindi wa kwanza kwa West Ham baada ya sare ya 1-1 ugenini na AFC Bournemouth, wakati Chelsea inapoteza mechi ya kwanza baada ya sare ya 1-1 nyumbani na Liverpool.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST HAM YAICHAPA CHELSEA 3-1 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top