MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki kambini kwao, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Clement Mzize, Crispin Ngushi mawili, Mburkinabe Stephane Aziz Ki, Mghana Hafiz Konkoni na Muivory Coast Peodoh Pacome Zouzoua.
Huo unakuwa mchezo wa tatu wa kujiandaa na msimu kwa Yanga chini ya Kocha mpya, Muargentina Miguel Ángel Gamondi baada ya kuzichapa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini 1-0 na Magereza ya Dar es Salaam 10-0.
0 comments:
Post a Comment