• HABARI MPYA

  Thursday, August 17, 2023

  SIMBA SC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 4-2 PALE PALE MANUNGU


  TIMU ya Simba imeanza vyema Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Othos Baleke dakika ya tano na viungo, Mcameroon Willy Essomba Onana dakika ya tisa, Mkongo Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 45 na Mzambia Clatous Chotta Chama dakika ya 81.
  Kwa upande wa wenyeji, Mtibwa Sugar mabao yote yamefungwa na mshambuliaji wao mpya, mzawa Matheo Anthony Simon dakika ya 20 na 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 4-2 PALE PALE MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top