// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAANDALIZI YA UZINDUZI WA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE YAANZA RASMI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAANDALIZI YA UZINDUZI WA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE YAANZA RASMI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, August 07, 2023

    MAANDALIZI YA UZINDUZI WA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE YAANZA RASMI


    KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amepokea ugeni wa timu ya wataalam wa African Football League chini ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili kuanza maandalizi ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Oktoba 20, 2023 jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza mara baada ya ziara ya ukaguzi wa maeneo ambayo yatafanyiwa ukarabati ili kuendana miongozo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Agosti 7, 2023 jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu, Yakubu amesema mazungumzo yao yalijikita zaidi kuangalia ubora wa Uwanja na maeneo ambayo yatafanyiwa ukarabati.
    “Mazungumzo yetu yalijikita zaidi pamoja na ziara ya uwanja kuangalia ubora wa uwanja na maeneo ambayo tunaenda kuyafanyia ukarabati na mahitaji yao kwa ajili ya mechi ya ufunguzi ambayo kwa bara zima la Afrika itafanyika hapa katika uwanja huu wa Benjamin Mkapa” amesema Katibu Mkuu, Yakubu.
    Mashindano  ya African Football League yanatarajiwa kuwa na manufaa mengi kiuchumi hapa nchini kwa kuwaleta wageni mashuhuri takriban 400 ambao watashiriki wakiwemo viongozi wa juu wa CAF na FIFA.
    Katibu Mkuu, Yakubu amesema wizara hiyo tayari imeshaingia mkataba na mkandarasi mkandarasi  wa ukarabati huo  Beijing Construction Engineering Group Co., Ltd. (BCEG) na kusisitiza kuwa mkandarasi huyo amekabidhiwa rasmi uwanja ili aendelee na majukumu yake ya ukarabati.
    Ukarabati wa awali utajumuisha masuala mbalimbali ambayo CAF wanahitaji yafanyiwe kazi mapema, baadhi yanagharamiwa ikiwa ni sehemu ya mkataba na baadhi ni gharama inayotolewa na CAF kwa ajili ya mechi hiyo ya ufunguzi ambayo itafanyika nchini.
    Kwa hivi sasa mpaka Oktoba 20, 2023 hakutakuwa na mechi nyingine itakayochezwa kwenye uwanja huu wa Benjamin Mkapa ili kupisha maandalizi kwa sababu miongoni mwa vitu watakavyofanya African Football League ni pamoja na kufumua eneo la kuchezea mpira kwa gharama zao na watalirejesha kwenye hali ambayo unachezeka mpira.
    Michuano hiyo inashirikisha vilabu nane kote barani Afrika  Simba ikiwemo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAANDALIZI YA UZINDUZI WA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE YAANZA RASMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top