• HABARI MPYA

  Wednesday, August 23, 2023

  YANGA SC YAANZA LIGI KWA KISHINDO, KMC YAFA 5-0


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuitandika KMC mabao 5-0 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na beki Dickson Job dakika ya 17, viungo Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 58, mshambuliaji Mghana Hafiz Konkoni dakika ya 69 na viungo Mzanzibari Mudathir Yahya dakika ya 76 na Muivory Coast Pacome Zouazoua dakika ya 80.
  Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga msimu huu, huku KMC wakicheza mechi ya pili baada ya sare ya 1-1 ugenini na Namungo FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA LIGI KWA KISHINDO, KMC YAFA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top