• HABARI MPYA

  Thursday, August 31, 2023

  CHELSEA WATINGA RAUNDI YA TATU KOMBE LA LIGI ENGLAND


  TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda ya Tatu ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AFC Wimbledon ya Daraja la Pili katika mchezo uliofanyika Uwanja wa  Stamford Bridge Jijini London  usiku wa jana.
  Haukuwa ushindi mwepesi kwa Vijana wa Kocha Muargentina,
  Mauricio Pochettino, kwani walilazimika kutoka nyuma kwa mabao ya Noni Madueke kwa penalti dakika ya 45 na ushei na Enzo Fernandez dakika ya 72 kufuatia AFC Wimbledon kutangulia na bao la James Tilley dakika ya 19 kwa penalti pia.
  Kwa ushindi huo, The Blues watakutana na wapinzani wa Ligi Kuu ya England katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, Brighton & Hove Albion Septemba 26 hapo hapo Stamford Bridge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA WATINGA RAUNDI YA TATU KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top