• HABARI MPYA

  Saturday, August 19, 2023

  SPURS YAIKANDA MAN UNITED 2-0 LONDON


  WENYEJI, Tottenham Hotspur wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao ya Tottenham Hotspur yamefungwa na kiungo Msenegal, Pape Matar Sarr dakika ya 49 na beki Muargentina, Lisandro Martínez dakika ya 83 huo ukiwa ushindi wa kwanza kwao baada ya sare ya 2-2 na Brentford ugenini.
  Kwa upande wao Manchester United leo wamepoteza mechi ya kwanza baada ya kuanza na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Wolverhampton Wanderers.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPURS YAIKANDA MAN UNITED 2-0 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top