• HABARI MPYA

  Sunday, August 27, 2023

  MAN CITY YAENDELEZA UMWAMBA LIGI KUU ENGLAND


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameendelea wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Sheffield United mabao 2-1 leo Uwanja wa Bramall Lane, Sheffield.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Erling Haaland dakika ya 63 na Rodri dakika ya 88, wakati la Sheffield United limefungwa na Jayden Bogle dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi tisa, huku Sheffield United ikibaki bila pointi baada ya wote kucheza mechi tatu za mwanzo za msimu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAENDELEZA UMWAMBA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top