// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TIMU YA WAKAGUZI CAF YAHITIMISHA UKAGUZI WAKE TANZANIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TIMU YA WAKAGUZI CAF YAHITIMISHA UKAGUZI WAKE TANZANIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, August 03, 2023

    TIMU YA WAKAGUZI CAF YAHITIMISHA UKAGUZI WAKE TANZANIA


    TIMU ya Wakaguzi ya utayari wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji AFCON 2027, kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imehitimisha ukaguzi wao salama Agosti 2, 2023 Zanzibar kwa kikao cha majumuisho kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Saidi Yakubu.
    Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amezishukuru Serikali za nchi hizo kwa ushirikiano waliotoa kufanikisha ukaguzi huo ikiwemo nia ya kuomba kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
    “Ukaguzi umemalizika vizuri, kwa kweli wameona tupo ‘serious’ na kuna mambo ambayo wametuelekeza tuyafanye, kwa upande wetu kama Tanzania bara na Zanzibar yapo mengi yamefanyika kwa sababu wakandarasi wapo site na vitu vinaonekana, wameelekeza hili jambo hili tulifanye kwa pamoja na wametoa siku 10 ili kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika kulingana na maelekezo yao” amesema Rais Karia.
    Aidha, Rais Karia ametoa rai kwa mataifa yote matatu kutekeleza kwa pamoja maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la Afrika Mashariki kuandaa mashindano hayo ambayo hayajawahi kufanyika katika ukanda huo na nchi hizo zinatakiwa kukamilisha miundombinu ya michezo itakayotumika kwenye mashindano hayo kabla ya Desemba 2025.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA WAKAGUZI CAF YAHITIMISHA UKAGUZI WAKE TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top