• HABARI MPYA

  Saturday, August 05, 2023

  AZAM FC YAICHAPA BANDARI YA MOMBASA 2-0 CHAMAZI


  MABAO ya beki Msenegal, Cheikh Sidibé na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube yameipa Azam FC ushindi wa 2-0 dhidi ya Bandari ya Mombasa nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Huo ni mchezo wa tano wa kujipima kwa Azam FC kuelekea michuano ya Ngao ya Jamii wiki ijayo Jijini Tanga baada ya awali kucheza mechi nne kwenye kambi yake ya mjini Sousse nchini Tunisia.
  Katika mechi hizo nne za Tunisia, Azam ilifungwa 3-0 na Esperance  3-1 na Stade Tunisien huku wao wakishinda mechi mbili, 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan na 2-1 dhidi ya wenyeji wengine, US Monastir.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA BANDARI YA MOMBASA 2-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top