• HABARI MPYA

  Wednesday, August 23, 2023

  CLARA LUVANGA WA YANGA ASAINI MIAKA MITATU KLABU YA HISPANIA


  MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya vijana ya wanawake Tanzania, Clara Cletus Luvanga amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Dux Logrono ya Hispania kutoka Yanga Princess ya nyumbani.
  Dux Logroño kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake, ambayo ni ya pili kwa ukubwa Hispania inayojulikana kama Reto Iberdrolana.
  Timu hiyo ipo chini ya kocha Gerardo García León, ambaye ni beki wa zamani wa kulia klabu za Villarreal, Valencia na Real Socieadad pamoja na timu C na B za Real Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CLARA LUVANGA WA YANGA ASAINI MIAKA MITATU KLABU YA HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top